Hali ya utulivu imeshuhudiwa katika eneo la Kayole Junction katika siku ya pili ya maandamano ya usafirishaji yaliyokuwa yakishuhudiwa eneo hilo.
Licha ya hali kutulia na biashara nyingi kuendelea kama kawaida, huduma za usafiri zimeendelea kutatizika huku wananchi wengi wakionekana barabarani wakingoja magari ya kuwapeleka katika shughuli zao za kila siku.
Baadhi ya wakazi wamesema wameathirika kutokana na kuchelewa kufika kazini pamoja na kutumia muda mrefu kusubiri usafiri. Hata hivyo, wafanyabiashara wameendelea na shughuli zao huku wakitumaini hali ya kawaida itarejea kikamilifu.

Kwa upande mwingine, hali ya usalama imeendelea kuwa shwari huku maafisa wa usalama wakionekana katika baadhi ya maeneo kuhakikisha amani inadumishwa.
Wakazi sasa wanatoa wito wa kupatikana kwa suluhisho la haraka ili huduma za usafiri zirejee kawaida na wananchi waweze kuendelea na shughuli zao bila usumbufu.
